
Mkurugenzi
wa Huduma Mbadala za Benki wa CRDB Joseph Witts akiongea na waandishi
wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya kutoa
pesa kwenye M-pesa kupitia ATM za benki bila kuhitaji kuwa na kadi wala
akaunti ya beki hiyo. Wengine pichani ni Ofisa Mkuu wa Biashara
Mtandao wa Vodacom Jacques Voogt na Meneje Uhusiano wa Nje wa Vodacom
Salum Mwalim.

Ofisa
Mkuu wa wa Biashara Mtandao wa Vodacom Jacque Voogt akittumia ATM ya
Benki ya CRDB kutoa pesa kwenye akaunti ya M-pesa katika simu yake ya
mkononi muda mfupi baada ya kuzinduliwa kwa huduma hiyo mpya. Kushoto
ni Mkurugenzi wa Huduma Mbadala za Benki wa CRDB Joseph Witts. Huduma
hiyo humuwezesah mteja yoyote wa M- pesa kutumia ATM za benki hiyo
kuchukua pesa bila kujali kama ni mteja wa CRDB.

Mkurugenzi
wa Huduma Mbadala za Benki wa CRDB Joseph Witts akitumia ATM ya Benki
ya CRDB kutoa pesa kwenye akaunti ya M-pesa katika simu yake ya mkononi
muda mfupi baada ya kuzinduliwa kwa huduma hiyo mpya. Kushoto ni Ofisa
Mkuu wa Biashara Mtandao wa Vodacom Jacques Voogt. Huduma hiyo
humuwezesha mteja yoyote wa M-pesa kutumia ATM za CRDB popote nchini
kutoa pesa hata kama si mteja wa benki hiyo.

Ofisa
Mkuu wa wa Biashara Mtandao wa Vodacom Jacques Voogt na Mkurugenzi wa
Huduma Mbadala za Benki wa CRDB Joseph Witts (katikati wenye suti
nyeusi) wakipongezana baada ya kuzindua huduma m-pya ya kutoa pesa
kwenye M-pesa kupitia ATM za CRDB nchi nzima. Wengine pichani ni
wafanyakazi wa Vodacom na wa Benki ya CRDB. Huduma hiyo huweza
kutumiwa na mteja yeyote wa M-pesa hata kama si mteja wa benki hiyo.
source: tanzaniatoday
No comments:
Post a Comment