AIRTEL YAZINDUA LUKU OFA KUPITIA HUDUMA YA AIRTEL MONEY
![]() |
Meneja Uendeshaji Kitengo cha Airtel Money Bwana Asupya Naligingwa akiongea wakati wa Uzinduzi wa ofa itakayowawezesha wateja wa Airtel kupata LUKU Bonus kupitia huduma ya Airtel Money |
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo
imezindua ofa mpya itakayowawezesha wateja wake kupata LUKU Bonus kila wakati
watakaponunua LUKU kupita huduma Airtel Money. ofi hii ni mwendelezo wa
dhamira ya Airtel katika kuhakikisha wateja wake wanapata huduma bora nchini.
Akiongea kuhusu ofaa hii Meneja wa kitengo cha
Airtel Money Asupya Naligingwa alisema“ ofa hii imelenga katika
kuwawezesha wateja kutumia huduma ya Airtel Money kununua Luku kwa
urahisi, usalama na haraka zaidi. Wateja wetu watapata LUKU unit s
bonus zao hapohapo pale watakaponunua luku kwa kupitia huduma ya Airtel
Money, Bonus hii wataipata mara nyingi kwa kadri watakavyonunua LUKU kwa siku.
Ofa hii inaendana na ulimwengu wa maisha ya kisasa kwani inaokoa muda na
kurahisha kufanya manunuzi kwa urahisi mahali popote na wakati wowote.
Natoa wito kwa wale ambao hawajawahi kutumia
huduma hii wafanye sasa“ kwani tuanishi katika ulimwengu ambao kutunza muda ni
muhimu sana”.
Bwana Naligingwa aliongeza kwa kusema huduma
hii ni kwa wateja wote wa Airtel nchi nzima hakuna haja ya kujiunga au
gharama yoyote kutozwa ili kufurahia Bonus kwa manunuzi ya LUKU kupitia
huduma ya Airtel Money.
“ili kupata huduma ya Airtel Money mteja
anatakiwa kupiga *150*60# na kuunganishawa na orodha ya Airtel Money
itakayokuwezesha kufanya miamala mbalimbali ikiwemo kununua LUKU.
Airtel Tanzania inatoa huduma ya fedha kwa
njia ya huduma ya Airtel Money ambapo imekuwa msaada mkubwa katika maisha ya
watanzania. Jitihada za kuwezesha upatikanaji wa huduma za Airtel
Money nchini umeendelea kuwa wa mafanikia ambapo Airtel imeweza
kuwa na mawakala wa Airtel Monye zaidi ya 35,000 nchin nzima na kuwezesha
upatikanaji wa huduma za kifedha na manunuzi ya bidhaa mbalimbali kuwa rahisis
na ufanisi zaidi. Huduma hii imekuja kwa wakati muafaka hivyo napenda
kuwahamasisha wateja kuendelea kufurahia huduma hii ya Airtel Money”.aliongeza
Naligingwa.
Huduma ya Airtel Money inawawezesha wateja
wake kufanya malipo ya ankra za bidhaa na huduma kama vile. DAWASCO, LUKU, USA
visa, DSTV, pamoja na kununua muda wa maongezi, kununua vifurushi vya
yatosha , kutuma na kupokea pesa kwa nusu gharama na Bure kupitia
vifurushi vya bure pack pamoja na huduma nyingine nyingi.
No comments:
Post a Comment