MKURUGENZI MKUU WA NHC AMTEMBELEA BALOZI MDOGO WA TANZANIA, DUBAI OFISINI KWAKE
![]() |
Mheshimiwa Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Ubalozi wa
Tanzania uliopo Dubai, akiwa na mazungumzo na Ndugu Nehemiah Mchechu,
Mkurugenzi Mkuu wa NHC , alipomtembelea Ofisini kwake Dubai.
|
Mazungumzo yao yalihusu maandalizi ya kongamano la
uwekezaji katika sekta ya nyumba litakalofanyika Jumeirah Madnat Hotel, Dubai.
Kongamano hilo limeandaliwa na Ubalozi Mdogo wa Tanzania uliopo Dubai kwa
kushirikiana na Shirika la Taifa la Nyumba (NHC).
Makampuni makubwa ya sekta ya nyumba hapa Dubai
pamoja na mengine kutoka Nchi za Muungano wa Ukanda wa Mashariki ya Kati (GCC
and the Midle East) yatashiriki. Makumpuni hayo ni pamoja na Nakheel ambalo
ndio limejenga The Palm City ya Dubai, Emaar ambalo ndio wamiliki wa Dubai
Mall. Mengine yanatoka Qatar, Bahrain, Oman na Saudi Arabia.
![]() |
Ndugu Nehemiah Mchechu (Kushoto) akiwa katika pamoja na Mheshimiwa Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Ubalozi wa Tanzania uliopo Dubai |
No comments:
Post a Comment