JAPAN YASAIDIA SERIKALI YA TANZANIA KATIKA KUINUA SEKTA YA KILIMO
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Serikali ya Tanzania imepokea msaada wa zaidi ya sh. bilioni sita (6) za Kitanzania ambazo ni sawa na Yen milioni 380 zilizotolewa na Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Kimataifa la Misaada (JAICA). Kauli hiyo ilitolewa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa kupokea msaada huo ambao utatumika kukuza sekta ya kilimo na kupunguza umasikini nchini. Katibu Mkuu Dkt. Likwelile alisema kuwa msaasa huo utatumika kununulia mbolea (UREA) ili kuongeza tija katika uzalishaji mazao na unalenga kuwafikia wakulima wadogo wadogo nchini ili kuwaongezea kipato chao.
Katibu Mkuu huyo alisema kuwa msaada huo umekuja
muda muafaka ambapo serikali inachukua hutua za makusudi kuinua sekta ya kilimo
ambayo inawaajiri watanzania takribani asilimia 74 nchini. Aidha,
Katibu Mkuu aliishukuru Serikali ya Japan kwa msaaada huo na kumhakikishia
Balozi wa Japan nchini Mh. Masaki Okanda kuwa msaada uliotolewa na Japan
kupitia JAICA utatumika kulinganana malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake Balozi wa Japan nchini
Masaki Okanda alisema kuwa msaada uliotolewa na Serikali yake kupitia JAICA
unalenga zaidi sekta ya kilimo na kusaidia kuimarisha miundo mbinu ya barabara
na masoko ambayo ndiyo kiini cha ufanisi katika sekta hiyo. Naye
Mwakilishi wa Mkuu wa JAICA nchini Yasunori Onishi alisema kuwa mahusiano
mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Japan ni wa kihistoria ulianzishwa tangu
mwakqa 1974 ambapo mkoa wa Kilimanjaro ulikuwa unanufaika na misaada hiyo
katika kuboresha kilimo.
Akimshukuru Katibu Mkuu Likwalile na Balozi wa Japan
nchini Okanda, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika
Yamungu Kayandabila alisema kuwa amefurahi Wizara yake kupata masaada huo na
ameahidi kuwa utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta kilimo chenye
tija nchini. Serikali ya Japan nchini kwa kushikiana na Tanzania katika
kusimamaia kilimo inaongozwa na nguzo kuu tatu ambazo ni kilimo, miundombinu na
utawala bora, hali ambayo itaihakikishia nchi kuwa na uhakika wa mazao bora na
hivyo kupunguza umasikini nchini.
No comments:
Post a Comment