Meneja
wa Upimaji toka Wakala wa Vipimo Bw. Richard Kadeghe akiwaonyesha
waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi ambavyo vipimo batili
vinayotumika.
Serikali yawatahadharisha wananchi kuhusu matumizi ya vipimo batili hususani visado na ndoo za Plastiki.
Hayo
yamesema na Kaimu Meneja wa Habari,Elimu na Mawasiliano wa EWakala wa
Vipimo Tanzania Bi Irene John wakati wa mkutano na waandishi wa habari
leo jijini Dar es salaam.
Akieleza
Bi Irene amesema ufungashaji na upimaji batili ni kinyume cha sheria ya
Vipimo sura 340 (iliyopitiwa mwaka 2002) pamoja na Kanuni zake.
Akifafanua
zaidi alisema ufungashaji na matumizi ya vipimo batili hudhoofisha
uchumi wa Taifa kwa kuwa humpunja mkulima,mlaji,mfanyabiashara na
mtumiaji.
Aliongeza
kuwa Serikali imekuwa ikipoteza mapato yake ambapo Halmashauri
hukusanya mapato pungufu wanapotoza ada kwa gunia badala ya uzito au
ujazo.
Irene alitaja
athari nyingine kuwa ni kuathiriwa kwa biashara ya kimataifa kutokana
na wananchi kutokuzingatia vipimo hasa kwa kutumia mizani wakati
wanapofanya biashara ya kununua na kuuza.
Naye
Mkurugenzi wa Idara ya ufundi wa wakala huo bw.Peter Masinga alisema ni
vyema wananchi wakaacha kutumia vipimo batili kwani vimekuwa
vikidhoofisha ukuaji wa uchumi kwa muda mrefu na hivyo kwenda kinyume na
jitihada za Serikali za kuwaletea maendeleo wananchi.
Bw.
Peter aliongeza kuwa kuanzishwa kwa vituo vya kununulia mazao vijijini
ni moja ya hatua zitakazosaidia kuondoa tatizo la vipimo batili kwa kuwa
Serikali itaweza kusimamia kwa ukaribu matumizi ya vipimo sahihi kama
vile mizani.
Wakala
wa vipimo ni Wakala wa Serikali ambayo ilianzishwa Mei,2002 kwa Tangazo
la Serikali namba 194 kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma bora kwa
wananchi, jukumu kuu likiwa kumlinda mtumiaji kupitia matumizi ya vipimo
sahihi.
No comments:
Post a Comment