Marmo Advert Banner

Royal Tughimbe Hotel

investment forum

investment forum

MACHEMBA STORE

MACHEMBA STORE

MBEYA SPRING WATER

MBEYA SPRING WATER

MADARAKA AUTO GARAGE

MADARAKA AUTO GARAGE

Friday, 25 April 2014

kampuni ya Tigo imeanza kushirikiana na Facebook

kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Tigo imeanza rasmi ushirikiano na mtandao wa kijamii wa facebook ambapo wateja wake wataweza kupata huduma za facebook kwa lugha ya kiswahili kupitia simu zake za mkononi, huduma itakayopatikana bila malipo.
mkurugenzi wa mtandao wa tigo Tanzania Diego Gutterez amesema, hii ni kwa mara ya kwanza kwa mtandao wa tigo kupatikana bila malipo katika eneo la Afrika mashariki. pia ni kwa mara ya kwanza kwa mtandao wa kijamii kama facebook kupatikana kwa kwa lugha ya kiswahili, na hii pia ni njia nzuri ya kuitangaza lugha ya kiswahili kimataifa.
akizungumza katika uzinduzi wa huduma hiyo Diego Gutterez amesema kwa mara ya kwanza wateja wa tigo wataweza kutumia mtandao wa facebook kwenye simu zao bila kukatwa gharama zozote hivyo kuwawezesha kuungana na wateja zaidi ya milioni mbili wanaotumia mtandao huo wa facebook hapa nchini.



mkurugenzi wa facebook wa ushirikiano na ukuaji kimataifa Nicola Delia na mkurugenzi wa wa tigo tanzania Diego Guterrez



No comments: