Marmo Advert Banner

Royal Tughimbe Hotel

investment forum

investment forum

MACHEMBA STORE

MACHEMBA STORE

MBEYA SPRING WATER

MBEYA SPRING WATER

MADARAKA AUTO GARAGE

MADARAKA AUTO GARAGE

Sunday, 13 April 2014

MATUKIO YA WIKI

 WAFANYABISHARA WAVUNJIWA VIBANDA VYAO VYA BIASHARA

Wafanyabiashara wadogowadogo jijini Mbeya waliokuwa wakifanya biashara zao pembezoni mwa barabara katika maeneo tofauti tofauti wamevunjiwa vibanda vyao usiku wa tarehe 11 April 2014.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya wafanyabiashara hao kukiuka agizo la manispaa lililokuwa likiwataka wafanyabiashara hao kuondoka katika maeneo hayo na kwenda kufanyia biashara zao katika maeneo maalum waliyotengewa na manispaa.
Hata hivyo, wafanyabiashara hao wamesema, sababu ya wao kutokwenda katika maeneo hayo ni kutokana na udogo wa eneo ikilinganishwa na idadi yao.
 " tatizo manispaa wametuambia tuhamie katika eneo ambalo ni dogo, ukiangalia sisi ni wengi sana na ukiangalia eneo wanalotuambia twende ni dogo, sasa tutafanyaje" mmoja wa wafanyabiashara hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Tumaini aliksikika akiongea.
Baadhi ya vibanda vililyovunjwa


Aidha, baadhi ya wafanyabiashara hao walisikika wakisema kuwa eneo wanaloambiwa wahamie si la serikali na kwamba eneo hilo ni la SIDO, hivyo wao hawatakiwi kuwepo hapo.
Eneo lingine walilotengewa wafanyabiashara hao ni Nanenane, lakini wafanyabiashara hao wamesema kuwa eneo hilo licha ya kuwa si sehemu nzuri kwa biashara kwa maana ya kwamba lipo sehemu isiyokuwa na mzunguko mkubwa wa watu  pia halijaandaliwa vizuri kwa ajili ya wao kufanyia biashara.
Hata hivyo, hatma ya wafanyabiashara hao itaamuliwa siku ya jumatatu tarehe 14 April 2014 watakapo kaa kikao na mamlaka husika.





No comments: