TAARIFA YA MAENDELEO YA UJENZI WA VITUO VYA UTOAJI WA HUDUMA KWA PAMOJA MIPAKANI (ONE -STOP BOARDER POSTS)
Mradi wa Vituo vya utoaji wa Huduma kwa Pamoja Mipakani (One-Stop Boarder Posts) unatarajiwa kurahisisha huduma mbali mbali zitolewazo mipakani ambazo ni kama vile forodha, uhamiaji, usimamizi wa ubora wa bidhaa, na ulinzi na usalama na kuzitoa upande mmoja tu wa mpaka kwa pamoja. Mradi huu umekwishakamilika kwa baadhi ya mipaka hapa nchini kama vile Holili, Mutukula na Sirari. Ujenzi wa Vituo vingine kama vile Namanga, Horohoro na Rusumo uko katika hatua za mwisho. Baada ya hapo Mradi huu utaendelea katika maendeleo mengine ya Mipaka kama vile Tunduma.
No comments:
Post a Comment