Kampuni ya mawasiliano ya simu za mikononi ya TIGO kupitia huduma yake ya TIGO PESA, imeanza kushirikiana na benki 17 nchini katika kutuma na kupokea pesa. katika huduma hiyo mteja anaweza kutuma pesa kutoka kwenye simu yake ya mkononi kwenda kweye akaunti ya benki, na pia kupokea pesa kutoka kwenye akaunti ya benki kwenda kwenye simu yake ya mkononi.
Bwana Andrew Hodgson mkuu wa huduma za kifedha wa tigo amesema kuwa, huduma hiyo iliyozinduliwa inatarajia kutimiza malengo ya kuwapatia wateja maisha ya kidigitali kwa kupata huduma za kibenki kutoka sehemu yoyote walipo kupitia simu zao za mikononi.
Aidha, kupitia huduma hii, wateja watapata usalama wa pesa zao ikiwa ni sambamba na kuepuka kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za kuweka na kupokea pesa.
![]() |
mkuu wa huduma za kifedha za tigo ndugu Andrew Hodgson (kushoto) na msemaji wa tigo ndugu John Mnyanja katika uzinduzi wa huduma hiyo |
No comments:
Post a Comment