Mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA) yafunga maduka makubwa (supermakets) 39 yaliyopo jijini Dar es Salaam.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya TFDA kubaini kuwa maduka hayo yamekuwa yakiuza vyakula hatarishi kwa afya na uhai wa watumiaji, bidhaa ambazo zimeingizwa kinyume cha sheria
Bidhaa zilizokamatwa ni pamoja na maziwa ya watoto makopo 591, makopo 1,526 ya vinywaji vya kuongeza nguvu, chumvi za kopo na paketi 6,090, vyote vikiwa na thamani ya takribani sh. milioni 30," alisema.
bidhaa zingine ni vinywaji vyenye ladha ya matunda, ambavyo havikidhi kanuni ya vielelezo, vimezuiliwa kutumika kwa lengo la kuchukua hatua zaidi ikiwa ni pamoja na kuviharibu.
TFDA ilifanya ukaguzi katika maduka 107 yaliyopo jijini Dar es Salaam kuanzia machi 10 hadi machi 21 mwaka huu. katika ukaguzi huo TFDA imebaini kuingizwa, kusambazwa na kuuzwa kwa vyakula, dawa na vipodozi ambavyo havikidhi viwango vya ubora
No comments:
Post a Comment