Marmo Advert Banner

Royal Tughimbe Hotel

investment forum

investment forum

MACHEMBA STORE

MACHEMBA STORE

MBEYA SPRING WATER

MBEYA SPRING WATER

MADARAKA AUTO GARAGE

MADARAKA AUTO GARAGE

Thursday, 20 March 2014

BIASHARA YA TAXI KABLA NA BAADA YA BODABODA

Biashara ya taxi ni miongoni mwa biashara maarufu sana za usafirishaji hapa nchini na kwingineko. kama zilivyo biashara zingine, changamoto mbalimbali hujitokeza katika biashara hii, kubwa zaidi ikiwa ni kupungua kwa mahitaji hasa kwa miaka ya hivi karibuni ambapo usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda umeshika kasi. ni kilio cha madereva taxi wengi kuwa kwa sasa biashara yao haipo kama ilivyokuwa miaka kadhaa nyuma ingawa wanajitahidi kuendelea kupambana.
Blog ya dailybusinesstz ilipata nafasi ya kuzungumza mawili matatu na mmoja wa madereva wa taxi wa jijini Mbeya katika kituo cha Sae bwana Godfrey Steven Ponella ambaye alikuwa na machache ya kuongea. yafuatayo ni mahojiano ya muda mfupi kati ya Godfrey na Dailybusinesstz (DBTz).
DBTz:  habari ya kazi bwana Godfrey
Godfrey: nzuri tu dada, karibu
DBTz: asante, bwana Godfrey unaweza kutuambia una uzoefu wa muda gani katika biashara hii?
Godfrey:  nina uzoefu wa miaka saba (7)
DBTz:  biashara ipoje kwa miaka ya nyuma na sasa?
Godfrey: kuna tofauti kubwa
DBTz: utofauti gani uliopo?
Godfrey: tofauti iliyopo ni kwenye mapato
DBTz: unadhani nini kinachangia kuwepo kwa tofauti ya mapato miaka ya nyuma na sasa?
Godfrey: kwanza abiria wengi wamenunua usafiri wao binafsi, na pili ni uwepo wa bodaboda na bajaj
DBTz: hapo kabla, mapato yalikuwaje?
Godfrey: ilikuwa ni kawaida kwa wiki ukapata shilingi laki mbili mpaka laki mbili na nusu
DBTz: na sasa hali ipoje?
Godfrey: unaweza ukapata kwa wiki shilingi elfu themanini, na ukipata sana elfu tisini, na kipindi hiki (kuanzia disemba mpaka machi) huwa ni kigumu sana, unaweza ukaambulia elfu sabini kwa wiki, hapo unakuwa umepata sana.
DBTz: unadhani nini kinachangia ugumu wa biashara katika miezi hiyo?
Godfrey:  sababu ni ada, na kilimo, miezi hii familia nyingi zinakuwa zinahangaika kwa ajili ya kuwalipia watoto ada, na wengine wanawekeza pesa nyingi kwenye kilimo.
DBTz: kila biashara ina changamoto zake, ina kanuni zake, ubunifu pia unahitajika katika kila biashara, wewe unawaambiaje madereva wanaofanya biashara hii ya taxi?
Godfrey: nachoweza kuwashauri au kuwaambia madereva wa taxi ni kwamba katika biashara hii, dereva anatakiwa awe jasiri, msiri, msafi, apende kazi yake, ajitume,  na lugha nzuri katika biashara.
DBTz: mnaathirika vipi na matukio?
Godfrey: tunazidi kuelimika, na sasa tuna kundi letu la Mbeya Taxi Group, polisi pia wanatuelimisha kila mara, na ikiwa umepakia mteja unayemtilia mashaka, basi unaweza kuwa unaendesha huku unatuma ujumbe mfupi wa maneno kutoa taarifa, tuna namba za simu za R.P.C mpaka ngazi ya chini kabisa.
Polisi wanatupa ushirikiano mkubwa sana, na sasa hivi wafanyabiashara ya taxi hawajihusihi katika matukio mabaya, wameelimika sana.
DBTz: unawaambia nini wateja wenu?
Godfrey: tupo kwa ajili yao, wakaribie
DBTZ: nashukuru sana kwa muda wako
Godfrey: asante, karibu sana.










Godfrey anasema abiria wanapenda gari nzuri, ni vizuri kutunza gari yako ya biashara

Godfrey Ponella akiwa kazini






1 comment:

Anonymous said...

Kwa upande wangu nimeendelea kuwa mteja wa taxi, i dont trust boda boda