MBEYA SPRING DRINKING WATER - Fahari ya Nyanda za Juu Kusini
Mbeya Spring Drinking Water ni wazalishaji wakubwa wa maji ya kunywa yanayowekwa kwenye chupa za kisasa jijini Mbeya. Licha ya kwamba maji haya huzalishwa jijini Mbeya, lakini yamekuwa yakiuzwa karibu kila mkoa katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambayo ni Mbeya, Iringa, Njombe, Ruvuma, Rukwa na Katavi. Ukuaji huu wa soko katika maji ya MBEYA SPRING DRINKING WATER kumechangiwa zaidi na sababu zifuatazo:
1. Maji haya yamekuwa yakiandaliwa kwa kuzingatia usafi na viwango vikubwa vya kimataifa. Ni kutokana na sababu hii, TFDA na TBS zimeweza kutambua na kutoa vibali kwa Kampuni ya KILANGI INVESTMENTS LIMITED ambayo ndiyo yenye dhamana ya kuzalisha, kupaki, kusambaza na kuuza maji haya
2. Maji yanayozalishwa na kupakiwa katika chupa yamezingatia taratibu nyingine kama vile tarehe ya kuzalishwa, tarehe ya kuisha muda (expiry date), anwani ya wazalishaji, jina la biashara (Brand Name/Trade Name), Batch Number au Code Number
3. Mitambo ya kisasa inayozashaji maji haya
4. Uongozi thabiti na wafanyakazi wenye utaalamu wa hali ya juu
5. Mazingira bora na safi ya uzalishaji
6. Magari ya kisasa ya usambazaji wa maji hadi kwa mtumiaji wa mwisho
Kutokana na mwitikio mkubwa wa watumiaji wa maji haya, kuna uwezekano mkubwa wa kupanua masoko yatakayojumuisha mikoa yote ya Tanzania na nchi jirani. Hivyo Kampuni ya KILANGI inakaribisha mawakala watakaokuwa tayari kusambaza huduma kwa wateja wengi zaidi.
Maji ya MBEYA SPRING DRINKING WATER huzalishwa na kupakiwa na chupa zenye ukubwa wa Lita 20, Lita 15, Lita 10, Lita 1.5 na Lita 0.5.
Mawasiliano yafanywe kwa kutumia:
Kilangi Investments Limited
Plot No. 23 Block U Soweto Area
P.O.
Box 2901, Mbeya – TANZANIA
Tel/Fax:
+255 25 2502131; Mobile +255-754 277081
Email:
madarakaautogarage@yahoo.com
No comments:
Post a Comment