UKANDA WA NYANDA ZA JUU KUSINI
WAVUTIA WAWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA UTALII NA MIFUGO
Meneja Kituo Cha Uwekezaji
Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Ndugu Daudi Riganda akitoa maelezo juu yakukua
kwa sekta ya uwekezaji katika Ukanda huo
Na Emanuel Madafa, Mbeya
HALI ya uwekezaji kwa Mikoa ya
Nyanda za juu Kusini, imetajwa kuridhisha kulingana na sekta mbalimbali ambazo
zinampa fursa mwekezaji kuamua kuwekeza eneo analo lihitaji
ikilinganishwa na kipindi cha nyuma kuanzia mwaka 2008.
Hayo yamesemwa na Meneja wa
uwekezaji Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Daud Liganda, ambapo amedai kuwa idadi
ya miradi iliyosajiliwa na kituo hicho imeendelea kukua hasa katika sekta
ya kilimo na ufugaji.
Amesema licha ya ukuaji huo kwa kasi
lakini bado umekuwa hauendani na hali
halisi ya maeneo husika hasa kutokana na kuwepo kwa mazingira mazuri ya
kiuwekezaji ambayo kama yakitumiwa vyema ukuaji huo utazidi kukuwa kwa kiwango
kizuri zaidi ukilinganishwa na kipindi hicho cha miaka mitano iliyopita. .
Amesema katika ukanda huo kuna
ardhi ya kutosha na yenye rutuba nzuri pamoja na mvua za mara kwa
mara zenye uwezo mkubwa wa kustawisha mazao ya aina yote.
Aidha Meneja huyo amedai kuwa licha
ya sekta za kilimo na ufugaji kukuwa kwa kiwango kizuri pia Sekta ya Utalii
nayo imezidi kupanda hasa katika ongezeko la ujenzi wa hoteli za
kisasa zenye hadhi ya kimataifa.
Pamoja na ongezeko hilo pia
meneja huyo amewataka wafanyabiashara wa ukanda huo hasa kwa mkoa wa
mbeya kuhakikisha wanaendana na uwepo wa uwanja wa kimataifa wa Songwe ambao
umetoa fursa kubwa hasa katika sekta ya utalii.
Ametaja fursa nyingine iliyopo
katika mkoa wa mbeya ni ya utoaji wa huduma za kijamii kama vile elimu na afya.
Amesema bado kituo hicho kinatoa rai
kwa wadau mbalimbali katika ukanda huo kuendelea kuchangamkia fursa hizo ili
kuweze kuendana na hali halisi ya ukuaji katika nyanja ya kiuwekezaji katika
ukanda huo.
Mwisho
1 comment:
Nina pongeza juhudi za Ndugu Daud ambazo ni za makusudi kabisa za kuwataka watanzania na hasa wafanya biashara wadogo na wakubwa wa mkoa wa Mbeya kuanza sasa kuchukua hatua za kuwekeza badala ya kufanya biashara pekee wakiwa hawana dira . Lakini wakati ndugu Daud anataka watanzania wa Mbeya kwenda hatua zaidi mbele na kuanza kuwekeza nashauri pia TIC waje na mpango shirikishi wa watu hawa wachanga katika mitaji .
Nashauri ndugu Daud atoke ofisini na kufanya maongezi na hawa watu uso kwa uso na awaeleze TIC Kanda inaweza kuwasaidia vipi kufikia malengo kwa ushirikiano .Mimi ninadhani wafanya biashara wadogo wadogo wakiwa na uelewa wa kutosha wanaweza kuwa rafiki mkubwa wa TIC . Lazima wajue kwamba TIC ina faida kubwa kwa wao na si kudhania kwamba ni kwa wageni pekee . Ndugu Daud nakupongeza kwa wito wako na kwa kuona kwamba ni wakati sasa wa mtanzania kipato cha kati kuwa mwekezaji na kushirikiana na TIC na kwa njia hiyo pia ajira itaongezeka Uchumi wa Nchi na hata kipato cha mtu mmojo mmoja kupitia uwekezaji mdogo mdogo.
Chukua hatua watembee na wakaribishe tengeneza familia ya TIC na iwe mfano kwa wengine .
Haya ndiyo maoni yangu kuhusiana na wito wako .
Post a Comment