Marmo Advert Banner

Royal Tughimbe Hotel

investment forum

investment forum

MACHEMBA STORE

MACHEMBA STORE

MBEYA SPRING WATER

MBEYA SPRING WATER

MADARAKA AUTO GARAGE

MADARAKA AUTO GARAGE

Friday, 14 March 2014

WITO WATOLEWA KWA WAWEKEZAJI KUTUMIA FURSA YA UWEKEZAJI JIJINI MBEYA

Meneja wa kituo cha uwekezaji Tanzania, kanda ya nyanda za juu kusini bwana Daudi Liganda atoa wito kwa wawekezaji kutumia fursa za uwekezaji mkoani Mbeya ipasavyo.
Akizungumza na blog ya dailybusinesstz, amewaasa wafanyabiashara na wawekezaji kuzitumia fursa zilizoko mkoani Mbeya katika kuongeza faida katika biashara zao.
                                                            Bwana David Liganda

   Meneja huyo  amezitaja fursa hizo kuwa ni, kilimo cha biashara, uanzishaji wa viwanda, ujenzi wa mahoteli na nyumba za biashara, biashara ya usafirishaji, huduma za jamii kama elimu na afya, pamoja na uanzishaji wa vituo vya radio na televisheni.
   Aidha amesema, endapo wafanyabiashra hao watajisajili na kituo cha uwekezaji, wanaweza kufaidika kwa kupewa punguzo la kodi katika vifaa watakavyovinunua kwa ajili ya miradi mbalimbali.
Hivyo basi kwa kufanya hivyo wanaweza kuokoa gharama kubwa ambayo ingetumika wakati wa kufanya biashara hizo.
wawekezaji hasa wa ndani wanashauriwa kuitumia ofisi ya kituo cha uwekezaji  nyanda za juu kusini kuweza kuendeleza biashara na miradi yao. ofisi hizo zinapatikana katika barabara ya Karume katika jengo la NBC linalotizamana na uwanja wa Sokoine.

No comments: