Kilimo cha korosho nchini kinatarajiwa kuchukua
sura mpya baada ya kutokana na kuwepo kwa mpango wa kujengwa kwa viwanda vitatu
vya kubangua korosho vitakavyoongeza thamani ya zao hilo. Lakini si hayo tu bali pia wakulima watanufaika
zaidi kwa kuwa korosho zitakuwa zikibanguliwa hapa nyumbani badala ya
kusafirishwa nje ya nchi zikiwa ghafi.
Akizungumza na gazeti la The Citizen, wiki
iliyopita, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania, Mfaume Juma alisema
viwanda hivyo vitajengwa katika Mkoa wa Mtwara, Wilaya ya Mkuranga na Tunduru
na vitaanza kazi mapema mwaka huu. Juma alisema fedha za ujenzi wa viwanda hivyo
zitatolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Korosho Tanzania, lakini hakufafanua
gharama za ujenzi. Mbali na hayo Juma anawataka wakulima kuandaa
vizuri kurosho ili wapate bei nzuri sokoni. “Kwa bahati mbaya, baadhi ya wakulima ambao si
waaminifu wamekuwa wakichanganya korosho na maji kwa ajili ya kuongeza uzito.
Tabia hii haikubaliki kabisa kwani inawakatisha tamaa wanunuzi na kushusha
thamani ya korosho yetu,” anasema mkurugenzi huyo.
Hivi sasa Tanzania inakadiriwa kubangua asilimia
mbili tu ya korosho yote nchini na kiasi kinachobaki kinauzwa nje kama mali
ghafi pamoja na kuwepo kwa mipango hiyo. Pamoja na kuwapo kwa mipango hiyo Tanzania
inatajwa katika Bara la Afrika kuwa katika nafasi ya pili kwa uzalishaji wa zao
hilo, ikifuatiwa na Nigeria. Lakini kilimo cha korosho kimekuwa kikikabiliwa na
matatizo mengi ambayo mpaka sasa hayajatatuliwa. Moja ya changamoto hizo ni ukosefu wa viwanda vya
kubangulia korosho na kusababisha wakulima kuuza korosho ambazo hazijabaguliwa.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na the
Agricultural Non State Actors Forum (ANSAF) mwaka 2008, kuuza korosho nje ya
nchi bila kubanguliwa kuna hasara zake kwani wakulima wamekuwa wakipata kipato
kidogo huku serikali ikikadiriwa kupoteza dola 110 milioni, kila mwaka. Utafiti
huo ulipewa kichwa cha habari. “Uboreshaji wa Mazingira ya Biashara ya Korosho
Tanzania”. “Vikwazo vya kujenga viwanda vya kubangua korosho
nchini, vimesababishwa na udhaifu wa sera, ukosefu wa fedha na kutokuwapo kwa
uzoefu katika soko la kimataifa,” sehemu ya utafiti, inaeleza.
Katika kipindi cha mwaka 2007 na 2012, zaidi ya
tani 461,000 za korosho ghafi ziliuzwa nje ya nchi kwa gharama ya dola ya Sh85
milioni sawa na Sh136 bilioni. Mtaalamu Mshauri wa kimataifa, Jim Fitzpatrick na
mwenye uzoefu wa miaka 30 katika zao hilo, anabainisha kuwa kutokuwapo kwa
mazingira mazuri ya soko ni moja ya matatizo yanayowaathiri wakulima wa
Tanzania. Fitzpatrick anaeleza kuwa wakulima wanaofanikiwa
kubangua korosho nchini, wamekuwa wakinufaika zaidi kuliko ambao wanauza
korosho ghafi nje ya nchi.
Kwa mujibu wa ripoti ya ANSAF, kama korosho ghafi
zilizouzwa nje nchi, zingeliuzwa zikiwa zimebanguliwa, wakulima wa korosho
wangepata dola 750 za Marekani sawa na Sh1.2 trilioni. Fitzpatrick anasema fedha ambazo wakulima
wanapokea ni kati ya asilimia 57 na 65 ya mauzo ikiwa ni bei halisi ya kuuzia
korosho huku wakipunjwa karibu asilimia 15 kutoka katika bei elekezi ya Bodi ya
Korosho.
“Gharama ya thamani ya korosho nchini haiendani
kabisa ukilinganisha na za nchi nyingine. “Kwa korosho inayouzwa India, mkulima anapata
kiasi kidogo, ukilinganisha na soko la kimataifa kutokana na kuwapo kwa gharama
kubwa za kodi, usafirishaji na gharama za wanunuzi wanaounua kwa mnada.
Kutokana na hali hiyo mkulima wa Tanzania hapati bei inayofanana na korosho
anayozalisha, ukilinganisha na wakulima wa Afrika Magharibi ambao soko lao liko
wazi,” anasema Fitzpatrick.
Kwa upande wake, Juma anasema malalamiko sugu
ambayo yalikuwa yakitolewa mara kwa mara, sasa yamepungua kutokana na usimamizi
mzuri wa zao hilo na kutoa elimu kwa wakulima. Kwa muda wa miaka minne sasa kumekuwapo kwa
malalamiko sugu kutoka kwa wakulima, kutokana na kutokuwapo kwa taarifa sahihi
za maendeleo ya zao hilo. “Kutokana na kanuni za mwaka 2009, mkakati wa
kutatua matatizo ya wakulima yako katika hatua ya utekelezaji. Licha kuwa na
wataalam wachache, kutokana na msaada wa bodi ya korosho, mambo yanakwenda
vizuri,” anasema Juma. Anasema hivi sasa kuna wilaya 42 zinazolima
korosho wakati nchi nzima ina wataalam 70. “Unategemea wataalamu wachache hivyo kukagua
wilaya zote 42? Wanaweza kufanya hivyo kama watapata msaada kutoka kwa wadau
wengine,” anasema.
Takwimu zinaeleza kuwa mahitaji ya korosho
duniani yanakuwa kwa asilimia 8 kila mwaka, ikiwa ni ishara kwamba Tanzania
inapaswa kuimarisha uwekezaji wa zao hilo.
HABARI KWA HISANI YA: shambanisolutions.blogspot.com
No comments:
Post a Comment